Mwalimu Daniel Urioh.
Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.

Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili  huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya kazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na sheria.  
 
Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji  hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.

Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza  hivi  shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania?

Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika.

Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.

Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania.  Shule hii huwatumia viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na  dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea kishahili na wanafunzi.

Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
Kwanza kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya waajiri.
Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.

Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za  watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza kuzifanya.

Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni  na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania. 
 
Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili. 
 
Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.

Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Kamanda kajunason inasikitisha sana nikiwa kama mwana blog stori hii tutawafikishia wana diaspora ili kuijadili zaidi, ila wakati naisoma nilitokwa na machozi na kujiuliza Tanzania tunakoelekea ni wapi...? Pole sana Mwalim ila tupo pamoja na wewe kuufikisha ujumbe huu kwa Wtanzania wote walio ughaibuni!

    ReplyDelete
  2. Nakushukuru sana mchangiaji kwa kuwakaripia hawa ndugu zetu wanaofanya kazi huko Marekani kwa kutokutambua uzawa kwanza.

    Kwanza kabisa kama ningekuwa mwanasiasa ningemuunga mkono mchungaji Christopher Mtikila na sera zake za uzawa. Nasema hivyo kwasababu wakati Mheshimiwa Mtikila anazungumzia Uzawa ni watanzania wachache sana waliomwelewa.

    Lakini ukweli wa neno hilo umetafriwa na msemaji aliyepita alipotoa mfano wa mwanafunzi wa udaktari anapokwenda kuchukua mafunzo katika nchi zinazotumia lugha tofauti na kiingereza.

    Amegusia uzawa kwa nchi hizo kutaka kujifunza lugha ya kwao kwanza. Mimi naenda mbali zaidi katika nchi kama marekani kama wewe ni daktari , mhasibu , au mtaalamu yoyote na umetoka Tanzania na vyeti vyako/ nondo kama wanavyoziita hakuna mahali popote utapata ajira kwa vyeti hivyo ni lazima uingie kwenye vyuo vyao

    Tumeona swala la ajira kwa wawekezaji kama alivyosema Urio kuwa familia nzima ipo kwenye menejiment bila kujali elimu walio nayo na serikali inakaa kama haioni. Angekuwepo Mtikila kwanza wakurugenzi wangekuwa wazawa wenye vyeti vinavyolingana na stahili ya uwekezaji huo.

    Kama alivosema urio watu wenye rangi nyeusi tumekuwa tunawaogopa watu wenye rangi nyeupe siyo tu hapo Tanzania hata huku ughaibuni wanafanya kama wao ni mungu watu kwa rangi nyeusi

    Pamoja na kuwa ni sekta binafsi ni lazima kuheshimu sheria za nchi zilizopo , na kama alivyosema mheshimiwa Raisi alivyokuwa anazungumzia raslimali za nchi hususan gesi ni wakati umefika sheria zitungwe kwa maslahi ya watanzania na sio wageni ili watanzania kunufaika na raslimali zetu katika secta zote, ziwe binafsi au serekalini

    Msemaji aliyepita amezungumzia mshahara duni ni kweli kwani hizo dola chache wanazolipa hazikidhi zaidi ya kulipa kodi ya chumba kama unataka maisha mazuzi zaidi ufanye kazi mbili hadi tatu na hatimaye kukaribisha kifo mapema kwa kukosa usingizi

    Serikali ikisimamia vizuri sekta binafsi hatimaye watanzania tulioko ughaibuni tutarudi nyumbani kuja kufanya kazi bega kwa bega na wawekezaji ili kujenga nchi yetu.

    Nchi hizi za ughaibuni zinapendeza kwa vile wameiba sana raslimali zetu ni wakati sasa kupinga kwa nguvu zote mipango mibovu ya uwekezaji wao kwani tumeshagundua janja yao

    Kwa kusimamia haki ni sharti mwalimu Uriyo arudishwe kazini na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wanahusika kwa aliyo yataja.

    Mungu ibariki Tanzania dumisha amani na upendo kwa watu wote wenyeji na wageni

    ReplyDelete
  3. Nakushukuru sana mchangiaji kwa kuwakaripia hawa ndugu zetu wanaofanya kazi huko Marekani kwa kutokutambua uzawa kwanza.