Dar es Salaam. Tarehe 6 Mei 2024: Benki ya CRDB imeandika historia nyingine kwa kupokea cheti cha kimataifa cha masuala ya mazingira baada ya jengo lake la Makao Makuu kukidhi vigezo vya kimataifa vya majengo yenye kuzingatia uhifadhi wa mazingira.

Cheti hicho cha kwanza kutolewa kwa majengo ya hapa nchini, kinatolewa na taasisi ya International Finance Corporation (IFC) ambayo ni kampuni tanzu ya Benki ya Dunia chini ya programu yake ya EDGE (Excellence in Design for Greater Efficiencies).

Akikabidhi tuzo hiyo, Mkuu wa Idara ya Majengo Yanayolinda Mazingira wa IFC, Dennis Quansah amesema ulinzi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na ni muhimu kuangalia kila kitu kinachochangia uchafuzi wa mazingira yanayoleta mabadiliko ya tabianchi na athari nyingine kwa viumbe viishivyo duniani.
“Ni furaha kwa IFC kulithibitisha jengo lenu kwamba linatunza mazingira. Hili ni jengo la kwanza kwa Tanzania. Cheti hiki tunachowapa ni utambulisho kwa taassisi na mashirika ya kimataifa yanayohamasisha utunzaji wa mazingira. Matumizi ya maji, nishati na vifaa vya ujenzi ni kati ya vigezo muhimu vinavyotumika kulitathmini jengo kabla ya kulithibitisha,” amesema Quansah.

Mkuu huyo amesisitiza kwamba Benki ya CRDB imeweka mfano unaopaswa kuigwa na taasisi nyingine nchini ili kuyaboresha majengo yao na kuunga mkono juhudi za kulinda mazingira na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

Cheti hicho ni uthibitisho wa juhudi za Benki ya CRDB sio tu yenyewe kulinda mazingira bali kuwezesha juhudi zinazofanywa na watu wengine kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kufadhili miradi yenye mrengo wa kulinda mazingira.
Sekta ya makazi ni kati ya maeneo yanayochangia uchafuzi wa mazingira kutokana na aina ya vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi wa nyumba, matumizi ya maji pamoja na nishati.

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema cheti hiki kinadhihirisha safari waliyoianza miaka mingi iliyopita hata wakawa taasisi ya kwanza ya fedha ukanda wa kusini na mashariki mwa Afrika kutambuliwa na Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (GCF) Novemba 2019.
“Kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya CRDB, ninafurahi kupokea tuzo hii ya kulitambua jengo letu la makao makuu kwamba linatunza mazingira tukikidhi vigezo kwenye vipengele vyote vitatu vinavyozingatiwa na IFC kabla ya kutoa cheti.

Tumepunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 21 na matumizi ya maji kwa asilimia 27. Vifaa tulivyovitumia kwenye ujenzi navyo vinapunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia 28 hivyo kutufanya kuwa juu ya kiwango cha chini kinachokubalika,” amesema Nsekela.

Akifafanua kuhusu vigezo hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Programu Endelevu wa Benki ya CRDB, Ramla Msuya amesema katika jengo la Benki ya CRDB, taa huzima zenyewe kama hakuna mtu ofisini na maji hayatoki iwapo hakuna mtu anayetaka kuyatumia.
“Taa zinatakiwa ziwake tu iwapo kuna mtu anahitaji mwanga na maji iwe maliwatoni au jikoni, yatatoka iwapo yanahitajika. Huwezi kukuta maji yanamwagika kwa kigezo kwamba mtu kasahau kufunga bomba, hapa kwetu bomba linajifunga lenyewe kama hakuna anayelitumia, hizi ni sifa ambazo hazipo kwenye majengo mengi nchini.

Vifaa vilivyotumika kweny eujenzi wa jengo hili ambalo Rais Samia Suluhu Hassan alilisifia wakati analizindua pia vinajali mazingira. Taka zote zinazokusanywa humu ndani zinarejelezwa, huwezi kuon ataka zimezagaa popote,” amefafanua Ramla.

Ili kuziwezesha taasisi na watu wengine wanaotaka kuyaboresha majengo yao yaendane na vigezo vya kimataifa vya kutunza mazingira, Nsekela amesema Benki ya CRDB inatoa mikopo inayoendana na malengo hayo.
“Tunao wabia zaidi ya 200 tunaoshirikiana nao kufanikisha uwezeshaji huu. Benki ya CRDB peke yake inaweza kukopesha mpaka dola milioni 107 za Marekani na ikishirikiana na GCF mkopo unafika dola milioni 250 na hakuna kikomo tukishirikiana na wabia wetu wengine.

Tunafanya hivi ili Tanzania nayo iwe miongoni mwa mataifa yenye miradi inayolinda mazingira. Mwaka jana tulitoa Hatifungai ya Kijani na kukusanya fedha nyingi kwa ajili ya miradi hii. Tunamkaribisha kila mwenye wazo au mradi wa kulinda mazingira,” amesema Nsekela.





Dar es Salaam, 3 Mei. Wadau wa sekta ya nishati wamedhihirisha nia yao ya kufadhili sekta ya usafirishaji katika harakati za kutunza mazingira kupitia gesi asilia nchini kwa wafanyabiashara wanaoendesha vyombo vya moto vya miguu mitatu, al maarufu kama bajaji.
Haya yamesemwa katika tukio la uzinduzi wa kampeni ya utunzaji wa mazingira chini ya kampuni ya Watu Credit (Tanzania) Limited ambayo imeanza kufadhili wafanyabiashara na bajaji zinazotumia gesi asilia, lengo likiwa ni kufadhili angalau bajaji 1,000 zinazoendeshwa kwa gesi asilia ifikapo mwisho wa mwaka 2024, na kuongeza kasi ya kuimarisha sekta ya usafirishaji katika matumizi ya vyanzo vya nishati safi.

Mpango huu ulizinduliwa rasmi mbele ya mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ambaye alisisitiza juu ya juhudi za ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ili kutimiza lengo la maendeleo endelevu la saba (7) linalohakikisha upatikanaji wa kupata nishati endelevu, safi na nafuu ifikapo mwaka 2030 kwa kila mtu.
Alinukuliwa, ‘tuko hapa leo kudumisha dhamira yetu ya wazi ya kukuza matumizi ya magari ya miguu mitatu yanayoendeshwa kwa gesi asilia (CNG) na hata yale yanayotumia umeme, na hivyo kupunguza utegemezi wa mafuta yanasobabisha ongezeko la hewa ukaa iletayo ongezeko la joto duniani huku sekta ya usafirishaji ikichangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira’.

Aidha, Mkurugenzi Mkaazi wa Watu Credit (Tanzania) Limited, Rumisho Shikonyi alisema, ‘Kuhamia kwenye nishati safi ni muhimu, na tumejitolea kufadhili mpango huu ili kuwasaidia abiria, madereva, na jamii kutumia usafiri safi, salama, na endelevu. Hii itatusaidia kulinda mazingira yetu kwa sababu mustakabali wa sayari yetu yote unategemea hatua tunazochukua leo’’.

Watu wamekuwa wakifanya kazi kuelekea lengo hili, wakifadhili bajaji zaidi ya 200 zinazoendeshwa kwa gesi asilia zenye thamani ya Tshs. bilioni 2.2 katika miezi miwili iliyopita pekee. Kampeni hii imelenga kufadhili angalau vyombo vya miguu mitatu 1,000 zaidi katika kutimiza azma yao ya kuboresha sekta ya usafiri barani Afrika.

Tukio hili pia lilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka sekta za nishati na mazingira, wakiwemo Mhandisi James Mologosho (Mhandisi Mkuu wa Gesi Asilia - Usambazaji na Ugavi kutoka EWURA), Tajiel Urioh, mtaalamu wa sera za mabadiliko ya tabia ya nchi, masoko ya kaboni na nishati safi, na Dkt. Esebi A. Nyari (Mhadhiri wa Uhandisi wa Mitambo na Mratibu wa Mradi wa CNG katika DIT).
Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning and Development wa Barrick Tanzania,Elly shimbi akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa kongamano lakuwajengea uwezo wakujiamini na kuhimili ushindani wa ajira na kujiajiri lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania lililofanyika katika chuo hicho mwishoni mwa wiki kwaudhamini wa Barrick.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo vya elimu ya juu mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Mayeka Simon Mayeka akiongea katika kongamano hilo.
Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya madini ya Barrick nchini, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma na Iringa lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika vyuo hivyo na kuwashirikisha wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu,wahadhiri na wadau mbalimbali.

Kupitia makongamano haya ambayo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira,kujiamini kwa kujiajiri,kuchangamkia fursa zinazojitokeza na kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Maofisa Raslimali Watu Waandamizi na wataalamu mbalimbali kutoka Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hayo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya dhahabu ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania,kuwezesha wanawake kuingia katika sekta na wafanyakazi wake.

Wanafunzi kutoka vyuo hivyo walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na ajira kwa wataalamu wa fani ya Raslimali kutoka makampuni mbalimbali walioshiriki katika makongamano hayo.

Akiongea katika kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Mayeka Simon Mayeka ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wanafunzi kujiamini wakati wote na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza zikiwemo za ajira na kujiajiri.
Alisema zama hizi na maisha ya kidigitali vijana wanayo nafasi kubwa kupata mafanikio iwapo wataandaliwa vizuri.Alipongeza taasisi ya AIESEC Tanzania kuandaa makongamano ya kuwajengea uwezo wanafunzi vyuoni pia aliipongezakampuni ya Barrick kwa kudhamini makongamano haya.
Wataalamu kutoka Barrick wakiongea katika kongamano la wanafunzi wa Chuo kikuu cha Iringa lililoandaliwa na na taasisi ya AIESEC Tanzania lililofanyika katika chuo hicho mwishoni mwa wiki kwa udhamini wa Barrick.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza katika Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa, akitoa Neno la Utangulizi wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024.
Baadhi ya washiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024.
Muwakilishi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo nchini (IFAD) Bi. JacquiIine Machangu Motcho, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024.
Baadhi ya washiriki, baada ya Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024.
Aliyeinama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, akiweka mbegu ya Samaki katika moja ya Bwawa, wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024.
Lipo la kujifunza katika utumishi wetu, Picha inajieleza, Kobra na Chatu kila Mmoja ni chanzo cha kifo Kwa mwenzake ingawa wote ni nyoka. Chatu kamuua Kobra Kwa kumyonga na Kobra kamuua Chatu Kwa kumng'ata. Mmoja kakosa hewa mwingine kadungwa Sumu na wote wamekufa. 

 Hivi ndivyo watu tunamalizana, urafiki unakwisha, mahusiano yanavunjika, familia zinasambaratika, taasisi zinakufa na kila upande kuumia kwa sababu ya kila Mmoja kutaka kuwa bora zaidi ya mwingine, wengine, kutaka kuoneshana umwamba au utemi! Wengine kuumizana kwa uzushi, umbea, kuwekeana maneno na kutengenezeana ajali, kuvuana nguo, kudhalilishana, kudhulumiana, ama kukwamishana kimajukumu mpaka wanaharibiana wote. 

Tafakari kabla ya kubeba dhamana ya kumfanyia mwenzako jambo la ovyo, tafakari dhamana yako na ya mwenzako kabla hamjafanyiana mambo yasiyo na tija. Tukumbuke, Sote tuna dhamana kila Mmoja kwa nafasi yake. 

Mwenyezi Mungu atusaidie kuyafahamu haya na kuyatenda kwa wema!
Na Munir Shemweta, MLELE

Mkazi wa kijiji cha Luchima katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile ametoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi.

Kiasi hicho cha pesa kimekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda tarehe 3 Mei 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luchima alipokwenda kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko katika jimbo lake la Kavuu.

‘’Nampongeza rais kwa vitendo kabisa naomba mhe, mbunge leo nikikabidhiwa fedha taslimu shilingi elfu tano umpelelekee Mhe, Rais ’’ alisema.

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, uamuzi wake unatokana na kuwiwa na uongozi bora na utendaji kazi wa Rais Samia hasa kwa kuwajali wananchi wa Luchima ambapo mbali na mambo mengine amewajali kwa kutoa fedha milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati aliyoieleza imewakomboa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda amesema atahakikisha kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na mwananchi huyo kinamfikia mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amempongeza mwananchi huyo wa kijiji cha Luchima wa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kama ishara ya kukubali juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Luchima na Tanzania kwa ujumla.

Amewaaleleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, Rais Samia anawapenda sana na amekuwa akisaidia juhudi mbalimbali za maendeleo kwenye jimbo la Kavuu na kutaja baadhi ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kutoa fedha za ujenzi wa hospitali, shule, barabara pamoja na upatikanaji wa huduma za maji.Mhe, Pinda amefanya ziara katika jimbo lake la Kavuu kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na kuathiri miundiombinu ikiwemo madaraja.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.Mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile akizungumza mara baada ya kumkabidhi shilingi elfu tano Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 3 Mei 2024.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.
Na Munir Shemweta, MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kauu Mhe, Geophrey Pinda ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara wa eneo Majimoto katika halmasauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Mhe, Pinda ametoa kauli hiyo tarehe 3 Mei 2024 wakati wa kikao cha pamoja kati ya Maafisa wa TRA Makao makuu na wafanyabiashara wa eneo la Majimoto kilichofanyika katika halmashauri ya Mpimbwe.

Kikao hicho cha siku moja kinafuatia kuwepo malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na maafisa wa TRA katika eneo hilo jambo walilolieleza kuwa limekuwa likisababisha usumbufu katika biashara zao.

‘’Mimi kama mbunge wa jimbo la Kavuu niko tayari kutoa ushirikiano na TRA lakini ushirikiano huo uende sambamba na mamlaka hiyo kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara ‘’ amesema Mhe, Pinda

Amesema, ni wajibu wake kuhakikisha maisha ya wafanyabiashara katika eneo la Majimoto yanakuwa rafiki na kusisitiza kuwa, eneo hilo linapoteza wateja wengi na sababu kuwa na mahusiano mabovu na walipa kodi.

Aidha, Mhe, Pinda amewataka maafisa wa TRA katika eneo hilo kutokuwa na dharau kwa wafanyabiashara na kuhoji unapomdharau mlipa kodi unategemea kitu gani huku akisisitiza mamlaka hiyo kutoa huduma nzuri kwa kwa wateja.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo wa jimbo la Kavuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania lazima maafisa wake wawe rafiki na wafanyabiashara ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kupeleka mkwamo kwa wafanyabiashara.

Amebainisha kuwa, TRA pamoja na mambo mengine lazima ijikite kutoa elimu kwa mlipa kodi kama ambavyo maafisa wake walivyofanya kwa kwenda kwa wafanyabiashara wa Majimoto huku akiwataka maafisa hao kuacha kabisa siasa katika shughuli za kibiashara. ‘’Nasema haya ili mje na mageuzi makubwa kwa lengo la kuboresha’’. Amesema Mhe, Pinda

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Daud amesema, zaidi ya asilimia hamsini ya mzunguko wa fedha katika halmashauri yake inatoka eneo la Majimoto na ndiyo maana halmashauri yake imeweka uwekezaji mkubwa katika eneo hilo ili kuhakikisha huduma za jamii zinaimarishwa na kupunguza changamoto kwa watu wanaoingia na kutoka eneo hilo.

‘’Kwa hiyo tunashukuru na tunatumaini kikao hiki watu watakapotoka watakuwa wamejifunza na TRA watakuwa wameelewa changamoto za maeneo hayo na kuwaletea mabadiliko makubwa’’. Amesema Mhe, Pinda.
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024.Mkuu wa Wilaya ya Mlele Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati wa kikao cha Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey PindaMkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Daud akizungumza katika kikao Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mlele Alhaji Majid Mwanga na kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Daud.



Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyabiashara wa eneo la Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 3 Mei 2024

 


Na Munir Shemweta, MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda amekabidhi baiskeli za walemavu wa miguu ikiwa ni jitihada za kuwasaidia watu wenye ulemau.

Mhe, Pinda amekabidhi baiskali tarehe 2 Mei 2024 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kirida katika Kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi.

Baiskeli iliyokabidhiwa kwa mlemavu Bi. Adela John mkazi wa Kirida ni sehemu ya baiskeli nne zilizotolewa kwa walemavu wa miguu wa jimbo la Kavuu ikiwa ni njia ya kuwasaidia usafiri wa kuwawezesha kwenda maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hiyo, Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Pinda amesema kuwa, anatambua adha wanayoipata walemavu wa miguu katika jimbo lake ndiyo maana ameona ipo haja ya kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kwenda katika shughuli zao.

‘’Ni matumaini yangu kuwa baiskeli hii itakuondolea adha uliyokuwa ukiipata na kwa sasa itakusaidia sana wakati wa kwenda katika shughuli zao mbalimbali’’ alisema Mhe, Pinda.

Mapema kwenye mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi, Mhe, Pinda aliwaeleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, pamoja na kukabiliwa na majukumu ya uwaziri lakini amekuwa akifanya juhudi ya kuwatumikia katika kuwaletea maendeleo.

Amezitaja juhudi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, zahanati na vituo vya afya, madaraja na shule za msingi na sekondari sambamba na upatikanaji huduma za umeme na maji.

‘’Pamoja na kwamba hamnioni mara kwa mara nikija hapa Kirida kutokana na majukumu niliyo nayo lakini nimekuwa nikifanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo na haya maendeleo mnayo yaona kama vile ujenzi wa bararbara, shule, zahanati na vituo vya afya, zote ni jitihada ambazo ninazifanya’’. Alisema Mhe, Pinda.

Awali wananchi wa Kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba walimueleza mbunge wa jimbo hilo kuwa wanakabiliwa na changamoto malimbali ikiwemo kutofanyika vikao vya kijiji kwa ajili ya kujua mapato na matumizi, kuwekewa alama za mipaka maeneo ya nyumba zao kwa madai kuwa makazi hayo yapo kwenye kingo ya mto na hivyo kutakiwa kuhama wakati mto ndiyo umehama.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda (Kushoto) akimkabidhi Baiskeli Mlemavu wa Miguu Bi. Adela John wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kidira katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mei 2, 2024. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba wakimuangalia Bi. Adela John ambaye ni mlemavu wa miguu mara baada ya kumkabidhi baiskeli tarehe 2 Mei 2024. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake katika jimbo la Kavuu Mei 2, 2024.
Beda Andrea mkazi wa kijiji cha Kirida Kona akiwasilisha changamoto zake kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kirida kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe Mei 2, 2024.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (Hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadahara uliofanyika kijiji cha Kirida Mei 2, 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)